Rushwa ya ngono inapunguza tija, ufanisi na nguvu kazi - TAWJA

Mwenyekiti wa Chama cha Majaji  Wanawake Tanzania (TAWJA), Jaji Engera Kileo, amesema tatizo la rushwa ya ngono linapunguza tija, ufanisi na nguvu kazi kazini, hivyo wadau wote wamewataka kushirikiana katika kupambana na kutokomeza vitendo hivyo.
Kauli hiyo aliitoa wakati alipokuwa akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo, majaji, polisi, nahakimu, magereza, wasomi wa vyuo vikuu na viongozi wa madhehebu ya dini kwenye wa semina ya inayo wahusu viongozi
na watekelezaji wa sheria juu ya mapambano dhidi ya rushwa ya ngono.

Jaji Kileo alisema tatizo la rushwa ya ngono ambalo limekuwepo kwenye
taasisi mbalimbali si tu linapunguza ufanisi basi linapunguza usawa na haki
na wakati mwingine inasababisha watu wasio na sifa kupata ajira na hata madaraka huku wale wenye sifa wakibaki kuwa nyuma.

Alisema  sasa chama hicho kinaendesha programu ya ‘sectortion’ ambao ni
msemo mpya wa kiingereza unaotumika kuelezea dhana ya matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono.

Jaji Kikeo alisema matumizi mabaya ya madaraka yanayohusisha rushwa ya ngono yanaweza kujitokeza sehemu zote za kazi na maa nyingi watu huogopa kukataa jambo lenye mahusiano ya kingono na viongozi wenye madaraka juu yao kwa kuhofia kupoteza ajira au nafasi nuri kazini kwa stahili zao.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa, amewataka majaji, mahakimu, wabunge kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia kiapo chao.

Alisema wabunge wanapotunga sheria kwa kuzingatia maslahi ya wananchi wafahamu kuwa wanatekeleza sheria kwa kuwa watafanya kazi hizo kwa weledi na hapo kwa upande wa umma unaweza kuwa na imani na mihimili hiyo ya serikali.

Galawa alisema kazi wanazozifanya ni muhimu sana katika kukuza na kuendeleza haki za binadamu katika taifa.

Alisema taifa lolote linastawi kiroho, kiuchumi na kijamii pale ambapo haki
inatawala, majaji, mahakimu na vyombo vinginevyo vya kisheria vinapotekeleza wajibu wao kwa kuzingatia kiapo chao haki lazima ipatikane.
SOURCE: NIPASHE JUMAPILI

Post a Comment

أحدث أقدم