Kufuatia
kuripotiwa kwa taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na
mgogoro wa mpaka uliokuwepo kutokana na madai kuwa kisiwa cha Pemba ni
sehemu ya Kenya, Serikali ya Tanzania imetoa taarifa rasmi kuhusiana na
mgogoro huo.
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe, amewatoa hofu
Wananchi kuwa Pemba ni sehemu ya Tanzania na hakuna ukweli wowote kwamba
kisiwa hicho ni sehemu ya Kenya.
Akijibu
kuhusiana na suala hilo Bungeni Dodoma leo Membe amesema; “Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijapata taarifa zozote rasmi kutoka
Serikali ya Jamhuri ya Kenya kuhusu mgogoro wa mpaka kati ya Serikali
hizi mbili… hususan madai ya kisiwa cha Pemba kilicho ndani ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ni sehemu ya Jamhuri ya Kenya.. Kisiwa cha Pemba
ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kitaendelea kubakia
hivyo daima…”

“Wizara
yangu iliwasiliana na ubalozi wetu Kenya lakini pia tuliwasiliana na
Serikali ya Kenya yenyewe.. kucheki kama taarifa hizi zilizoandikwa
kwenye magazeti zina mshiko wa Serikali, balozi wetu na serikali yenyewe
ya Kenya hawajui suala hili limetokea wapi” –Membe
Kuhusiana
na taarifa za kuwepo meli za kutoka Kenya zinazofanya shughuli za uvuvi
katika eneo la Tanzania, Membe amesema; “nitawasiliana na wenzangu
wanaohusika.. kuanzia wizara inayohusika na JWTZ ambao ndio wana dhamana
ya kulinda bahari yetu ya Indian Ocean waone namna ya kudhibiti na
namna ya kuwahakikishia wenzetu wa Kenya kwamba hata baharini kuna
mipaka yake”-Membe

Jaku
Hashim Ayoub, mbunge wa Baraza la wawakilishi Zanzibar akiuliza swali
kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
إرسال تعليق