
Mrembo wa Taifa mwaka jana 'Redd's Miss Tanzania 2013', Happiness Watimanywa.
Akizungumza na NIPASHE Ijumaa kabla ya kuondoka, Watimanywa alisema amejiandaa vizuri kwenda katika shindano hilo la dunia, lakini anaamini kuna 'wingu' limetanda kwenye vichwa vya Watanzania kwa sasa mara wanaposikia mshiriki wa taji hilo anafanya jambo lolote.
Watimanywa alisema kutokana na sakata la Sitti, ana jukumu zito la kuwashawishi wadau wa sanaa ya urembo kuweka mawazo yao pembeni na kumpa ushirikiano yeye ambaye amekwenda kupeperusha bendera ya Tanzania mwaka huu.
Alisema anaondoka nchini akiwa anajiamini hivyo Watanzania watarajie matokeo mazuri kutoka kwake.
"Lile ni shindano, naenda kushindana, ila naona watu wanasahau kama mimi naenda kushiriki mwaka huu na akili na mawazo yako kwa Sitti, sijui kama watanipigia kura au 'watacomment' kuhusiana na sakata ambalo lipo, naomba wabadilishe mawazo na wahamie upande wangu," alisema Watimanywa (20).
Mrembo huyo ambaye amezaliwa mkoani Tabora, alisema akiwa kwenye mashindano hayo amejiandaa vema kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyoko nchini na kwa kufanya hivyo Tanzania itaendelea kujulikana na yeye akijitangaza.
"Mimi naamini kila mmoja anaweza kupata mafanikio, kinachotakiwa kufanywa ni kuwa wewe kama wewe na si kuiga uhalisia wa mtu mwingine," Watimanywa aliongeza.
Alisema yuko tayari kukabiliana na changamoto na ushindani kwenye mashindano hayo ya kimataifa na kamwe hahofii washiriki wenzake.
"Najua tutakuwa warembo zaidi ya 130, ndiyo maana nimesema naenda kushindana na unapokwenda kushindana ni lazima uwe umekamilika, nimejifunza mambo mbalimbali na sana warembo waliopita wameniambia niondoe hofu, hofu itaniondolea hali ya kujiamini," alisema Watimanywa.
Aliitaja Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), kuwa imemsaidia katika maandalizi yake kwa kushirikiana na Kamati ya Miss Tanzania ambayo iko chini ya Hashim Lundenga.
CHANZO:
NIPASHE
إرسال تعليق