Shahidi huyo, Rosemary Kachungira, ambaye ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Equity Aviation aliieleza Mahakama kuwa,
alipokea baruapepe kutoka kwa Taasisi ya Based Hopes International,
ikiwataka waandae mitambo kwa ajili ya kupakia mizigo kwenye ndege.
Rosemary alisema, kutokana na kampuni yao
kushindwa kubeba mzigo huo, ilitoa kazi hiyo kwa Swissport na ndiyo
iliyopakia mzigo huo kutokana na mitambo ya Equity kubeba tani 40 tu.
Shahidi huyo aliieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kilimanjaro kuwa haikujua ni mzigo wa aina gani uliokuwa ukisafirishwa
kutokana na maombi ya baruapepe kueleza kuwa mzigo huo utapakiwa kama
‘diplomatic’.
Alikuwa akitoa ushahidi wake akiongozwa na Wakili
wa Serikali, Evetha Mushi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Simon Kobero.
Shahidi wa 32 Charels Mlokos, ambaye ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Wanyamapori, aliieleza mahakama hiyo kuwa,
mshtakiwa wa pili, Hawa Mang’unyuka, hakuwa na kibali cha kusafirisha
wanyama nje ya nchi.
- Mwananchi
- Mwananchi
Post a Comment