‘Swissport ndiyo iliyopakiza twiga hai’

Moshi. Shahidi wa 31 katika kesi ya kutorosha wanyama hai wakiwamo twiga wanne kwenda Uarabuni kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ameitaja Kampuni ya Swissport ndiyo iliyohusika na kazi ya upakiaji wanyama hao.
Shahidi huyo, Rosemary Kachungira, ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Equity Aviation aliieleza Mahakama kuwa, alipokea baruapepe kutoka kwa Taasisi ya Based Hopes International, ikiwataka waandae mitambo kwa ajili ya kupakia mizigo kwenye ndege.
Rosemary alisema, kutokana na kampuni yao kushindwa kubeba mzigo huo, ilitoa kazi hiyo kwa Swissport na ndiyo iliyopakia mzigo huo kutokana na mitambo ya Equity kubeba tani 40 tu.
Shahidi huyo aliieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kilimanjaro kuwa haikujua ni mzigo wa aina gani uliokuwa ukisafirishwa kutokana na maombi ya baruapepe kueleza kuwa mzigo huo utapakiwa kama ‘diplomatic’.
Alikuwa akitoa ushahidi wake akiongozwa na Wakili wa Serikali, Evetha Mushi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Kobero.
Shahidi wa 32 Charels Mlokos, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Wanyamapori, aliieleza mahakama hiyo kuwa, mshtakiwa wa pili, Hawa Mang’unyuka, hakuwa na kibali cha kusafirisha wanyama nje ya nchi.
- Mwananchi

Post a Comment

أحدث أقدم