Wataalamu wa afya kutoka Zahanati ya Mitwero
walisema hayo jana walipokutana na timu ya Shirika la Elizabeth Glaser
Pediatric Aids Foundation (EGPAF).
Muuguzi Grace John na Mganga Mfawidhi wa zahanati
hiyo, Ally Daudi walisema baadhi ya wanaume hukataa kupima afya zao pale
wanapoombwa na wake zao ili waweze kufahamu kama wapo salama au la.
Dk Daudi alisema kutokana na hali hiyo wanawake
huchukua uamuzi wa kupima VVU na kama wakigundulika wameathirika,
hunyamaza kwa kuhofia kupewa taraka.
“Hivi ninapozungumza na ninyi leo hii kuna mama
mmoja alimweleza mumewe wakapime ili kutambua afya zao, mume
alimkatalia, lakini mwanamke huyu alipokuja na kubainika ana VVU,
tulimuanzishia dawa.
“Lakini akasema atalazimika kuzificha chini ya ndoo ya maji ili asiachwe na mumewe,” alisema Dk Daudi.
Muuguzi John alisema alishawahi kusuluhisha ugomvi
wa wanandoa wawili, waliofika kupima afya zao na mwanamke
aliyegundulika kuwa na VVU huku mwanamume akiwa hana.
“Baada ya wanandoa hao kufika hapa kupima afya
zao, mwanamke alikutwa na maambukizi, lakini mwanamume hakuwanavyo,
kulitokea vuta nikuvute, mwanamume alikwenda dukani kununua karatasi na
peni kutaka kumwandikia mkewe talaka mbele yangu,” alisema.
Alisema kutokana na jitihada za kusuluhisha ugomvi huo, wanandoa hao walifanikiwa kupatana na kuweza kurejea nyumbani kwao.
- Mwananchi
- Mwananchi
إرسال تعليق