CHAMA Cha Afya ya
Jamii Tanzania (Tanzania Public Health Association-TPHA), kinajenga jengo la
kitega uchumi la kisasa la ghorofa 20, katika makao makuu ya chama hicho jijini
Dar es Salaam kama sehemu ya kujiongezea wigo wa mapato.
Hayo yalibainishwa kwenye
kongamano la 31 la Kisayansi na Mkutano mkuu wa mwaka wa TPHA unaoendelea
katika ukumbi wa Stella Maris, mjini Bagamoyo.
Tayari wataalamu wa
majengo nchini wa kampuni ya K&M Archplans (T)Ltd, wamewasilisha
mpango kazi wao huo ikiwemo mchoro wa jengo hilo la TPHA litakavyokuwa.
Wataalamu hao wa
K&M Archplans, kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,
Profesa Arch Livin Mosha alisema kampuni yao imebobea katika ukandarasi
wa majengo mbalimbali ikiwemo kuwa na uzoefu wa kutosha katika usanifu na
mpanilio wa majengo.
Jengo hilo
linatarajiwa kujengwa makao makuu ya TPHA, yaliyopo Kinondoni, mkabara na
barabara ya Ally Hassan Mwinyi (Barabara ya zamani ya Bagamoyo), Victoria
Makumbusho, jijini Dar es Salaam.
Naye Mwenyekiti wa
TPHA Taifa, Dk.Elihuruma Nangawe alieleza kuwa, Chama hicho kitaendela na
mchakato wake ikiwemo kujadiliana kwa kina na wanachama katika kufikia malengo
ya utekelezaji wake ambapo alibainisha kuwa lengo la TPHA, ni kujenga
jengo la gorofa 10 ama la gorofa 25.
Naye Katibu Mtendaji
wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga alisema kongamano hilo ni la
kuwakutanisha wataalamu ili kubadilishana ujuzi, uzoefu na kutoa
mapendekezo namna ya kuleta mabadiliko katika jamii hususani sekta ya afya hapa
nchini.
"Mpaka leo mada
mbalimbali za kitaalamu zimewasilishwa na wataalamu hao zikiwemo masula ya afya
ya msingi, jamii, Pia utafiti na mipngo juu ya magonjwa ya ukimwi,
kisukari, maendeleo ya afya mijini na vijijini na namna ya kuendeleza sekta ya
afya hasa kwa sekta binafsi na serikali" alisema Dk.Kisanga.
Kongamano hilo la
kisayansi lililoanza Jumatatu ya Novemba 24, wiki hii, linatarajia kumalizika kesho.
Source:Andrew Chale
Post a Comment