Video mpya ya Diamond platnumz ‘Ntampata wapi’ imekuwa na
mapokeo mazuri kiasi cha kuwavutia watu wengi kutaka kuitazama kila
wanaposikia kuwa imetoka.

Video hiyo iliyoanza kuchezwa na vituo vikubwa vya nje kikiwemo MTV
Base juzi kabla haijasambazwa kwenye vituo vya hapa nyumbani jana, mpaka
sasa imefanikiwa kupata views 117,907 kwenye mtandao wa Youtube, ikiwa
ni ndani ya saa 24 toka ipandishwe kwenye mtandao huo.
Post a Comment