Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kati ya
Tanzania na Ubelgiji,Otieno Igogo, akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa
Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza mara baada ya mkutano uliowakutanisha
wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Ubelgiji uliofanyika mjini
Bagamoyo. Wanaoshuhudia ni balozi wa Tanzania nchini humo, Dk. Deodorus
Kamala na Kamishna wa Biashara kutoka ubalozi wa Ubelgiji nchini, Ivan
Korsak (Picha na Mpiga Picha Wetu)
Taarifa za kupotea kwa kompyuta hizo zilitolewa jana na Balozi wa Tanzania Ubelgiji, Deodorus Kamala wakati wa ziara ya wafanyabishara kutoka nchini humo kwenye maeneo ya uwekezaji EPZ wilayani hapa.
Dk. Kamala alisema amesikitishwa na watendaji na viongozi wanaokiuka sheria katika utekelezaji wa majukumu yao na kuwakosesha wananchi fursa ya kupata maendeleo kutoka kwa wahisani wanaojitolea kuwasaidia.
Alisema kampuni hiyo ya Wakefield and Cushman kwa kushirikiana na Serikali imejenga shule hiyo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa mkoa wa Pwani na kutoa misaada.
Alisema kutokana na kompyuta kutofikishwa shuleni hapo, kampuni hiyo imesitisha kuisaidia shule hiyo kwa muda usiojulikana.
Kamalla alisema baada ya Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mwantum Mahiza (pichani) kuteuliwa kushika wadhifa huo mkoani Pwani, alimuita ofisini kwake na kumueleza kampuni hiyo kati ya fedha ilizoahidi kutoa, kilibaki kiasi hicho ambacho alitakiwa kufuatilia Ubelgiji.
“Juzi kabla ya kuja Tanzania nilikwenda ofisini kwao kujua wamefikia hatua ipi kumalizia hizo fedha zilizobaki nikaelezwa hivi karibuni walikuja nchini hadi sekondari ya Miono na kukuta imeanza na wamefurahi, lakini kompyuta walizotuma wamekuta hazipo kwa hiyo hawatatoa fedha hizo zilizobakia hadi kompyuta hizo zifikishwe shuleni hapo,” alisema.
Alisema walimwambia walipenda kuipatia kiasi hicho cha fedha shule hiyo kwa ajili ya matumizi mbalimbalim ikiwamo ya Internet na ya mawasiliano kwa mtandao wa kompyuta, lakini hawawezi kumpatia hadi kompyuta hizo zipelekwe shuleni hapo.
Alisema aliwaahidi akiwa nchini atazungumza na Mahiza, serikali na wizara ili kujua ziliko kompyuta hizo.
Kwa upande wake, Mahiza aliahidi kufuatilia wizarani ili kubaini kompyuta hizo ziliko na kuonya kama kuna ofisa alizipokea na kuziweka ofisini au kwenye shule nyingine, azisalimishe ofisini kwake lasivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
CHANZO:
NIPASHE
إرسال تعليق