SERIKALI imeobwa kulegeza masharti ya upatikanaji wa leseni za
kufungua kampuni ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa
vijana wanaohitimu mafunzo ya ufundi stadi (VETA).
Ombi hilo limetolewa mjini hapa juzi na wahitimu wa chuo hicho
wakati wa mahafali ya 38 chuo hicho ambao walisema hivi sasa ni vigumu
kupata ajira serikalini hivyo kutumia ujuzi wao kufungua kampuni
zitakazowapa ajira na kuwaletea maendeleo.
“Tunajivunia kumaliza kozi zetu ila changamoto kubwa iko katika
kupata ajira iwe serikalini ama taasisi binafsi kutokana na kuwa na
wasomi wengi ambao hawana kazi,” alisema Salim Ramadhani.
Kwa upande wake mkuu wa chuo cha ufundi stad veta Injinia Alfhonce
Rubasha alisema wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa madarasa
kutokana na ongezeko la wanafunzi.
Mkuu huyo wa Veta jijini hapa aliwaeleza wazazi na walezi kwamba
vyuo vya ufundi vinaweza kuwabadilisha watoto wao waliokosa nafasi ya
kuendelea na masomo katika mfumo rasmi hivyo kuwatambua kwa ujuzi wao.
Naye Ofisa Elimu Sekondari wa Jiji la Tanga, Bashiru Shelimo alisema
wapo wanafunzi wengi wanaomaliza sekondari wanakata tamaa na kusahau
kwamba vyuo vya ufundi vinaweza kuwatoa kimaisha kama vilivyo vyuo
vyengine.
- Tanzania Daima
إرسال تعليق