Wanahabari wawili wafariki dunia

Dar es Salaam. Tasnia ya habari imepata simanzi baada ya waandishi wawili wa habari, Innocent Munyuku na Baraka Karashani kufariki dunia jana jijini Dar es Salaam.
Taarifa za kifo cha Munyuku zilikuwa za kwanza kuitikisa familia ya wanahabari, baada ya kufikwa na mauti akiwa usingizini usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Kimara.
Kwa upande wa Karashani, ambaye ni mtoto wa mwanahabari mkongwe, Phiri Karashani, alifariki dunia jana mchana katika Hospitali ya Lugalo alikokuwa amelazwa tangu mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Absalom Kibanda, mhariri mtendaji mkuu wa New Habari, kampuni aliyokuwa akifanya kazi Munyuku kabla ya kifo chake, alisema mipango ya mazishi inafanyika na mwili wa marehemu utasafirishwa kesho kwenda Morogoro tayari kwa maziko Jumamosi. “Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Munyuku kwani alikuwa mwenzetu kwa siku nyingi. Hakika tutamkumbuka kwa mengi,” alisema na kuongeza kuwa kwa sasa msiba uko Mazimbu, Morogoro.”
Alisema kampuni inawasiliana na familia ya marehemu ili kutoa nafasi kwa watu kuaga mwili wa marehemu kesho kabla ya kusafirisha. Hadi kifo hicho cha ghafla, Munyuku alikuwa mhariri wa habari za siasa.
Munyuku pia aliwahi kufanya kazi Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd kama mhariri msanifu wa gazeti la Mwanaspoti.
Kwa upande wa Karashani, aliyewahi kufanya kazi New Habari kama mwandishi wa michezo wa magazeti ya Mtanzania, Bingwa na Dimba, msiba uko nyumbani kwa wazazi wake jirani na Kituo cha Daladala Simu 2000, nyuma ya jengo la Mawasiliano.
Kaka wa marehemu, Magezi Karashani alisema jana kuwa bado walikuwa kwenye vikao vya awali, hivyo ilikuwa vigumu kusema kama maziko yatafanyika jijini au watasafirisha

Post a Comment

Previous Post Next Post