Dar es Salaam. Tasnia ya habari imepata simanzi
baada ya waandishi wawili wa habari, Innocent Munyuku na Baraka
Karashani kufariki dunia jana jijini Dar es Salaam.
Taarifa za kifo cha Munyuku zilikuwa za kwanza
kuitikisa familia ya wanahabari, baada ya kufikwa na mauti akiwa
usingizini usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Kimara.
Kwa upande wa Karashani, ambaye ni mtoto wa
mwanahabari mkongwe, Phiri Karashani, alifariki dunia jana mchana katika
Hospitali ya Lugalo alikokuwa amelazwa tangu mwishoni mwa wiki
iliyopita.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Absalom
Kibanda, mhariri mtendaji mkuu wa New Habari, kampuni aliyokuwa akifanya
kazi Munyuku kabla ya kifo chake, alisema mipango ya mazishi inafanyika
na mwili wa marehemu utasafirishwa kesho kwenda Morogoro tayari kwa
maziko Jumamosi. “Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha
Munyuku kwani alikuwa mwenzetu kwa siku nyingi. Hakika tutamkumbuka kwa
mengi,” alisema na kuongeza kuwa kwa sasa msiba uko Mazimbu, Morogoro.”
Alisema kampuni inawasiliana na familia ya
marehemu ili kutoa nafasi kwa watu kuaga mwili wa marehemu kesho kabla
ya kusafirisha. Hadi kifo hicho cha ghafla, Munyuku alikuwa mhariri wa
habari za siasa.
Munyuku pia aliwahi kufanya kazi Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd kama mhariri msanifu wa gazeti la Mwanaspoti.
Kwa upande wa Karashani, aliyewahi kufanya kazi
New Habari kama mwandishi wa michezo wa magazeti ya Mtanzania, Bingwa na
Dimba, msiba uko nyumbani kwa wazazi wake jirani na Kituo cha Daladala
Simu 2000, nyuma ya jengo la Mawasiliano.
Kaka wa marehemu, Magezi Karashani alisema jana
kuwa bado walikuwa kwenye vikao vya awali, hivyo ilikuwa vigumu kusema
kama maziko yatafanyika jijini au watasafirisha
إرسال تعليق