Ni miaka minne sasa tangu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa
Kitaifa visiwani Zanzibar (SUK), ambayo kwa kiasi kikubwa imerejesha
siasa za kistaarabu, ushindani wa sera za vyama, amani na utulivu.
Salma Said, Mwananchii
Zanzibar. Licha ya kuwapo kwa maelewano
yaliyotokana na kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), kumekuwa
na mawazo tofauti kwa baadhi ya wanasiasa visiwani Zanzibar wakitaka
kurejea hali ya mwanzo na kuachana na muundo wa Serikali hiyo
iliyovishirikisha vyama viwili vikuu visiwani humo vya CCM na CUF.
Baadhi ya wanasiasa wanaukosoa mfumo wa SUK kuwa
hauna tija kwa siasa za Zanzibar, wengine wakiuelezea mfumo huo kuwa
umeiweka Zanzibar katika siasa za kileo za ushindani wa hoja.
Miongoni mwao wanataka kurejea hali iliyokuwa mwanzo ya siasa za ushindani wa nguvu na zisizo na maelewano.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa
Chama cha Mapinduzi na Mwakilishi wa viti maalum, Asha Bakar Makame,
mara kadhaa ametamka hadharani nia yake na ya baadhi ya wawakilishi
wenzake kutaka kuwasilisha hoja binafsi ili kuondokana na mfumo huo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mwakilishi wa Jimbo
la Magomeni, Salmin Awadh Salmin, naye anaipinga wazi wazi SUK na
kutamka dhamira yao ya kuwasilisha hoja binafsi kutaka Zanzibar irejee
katika mfumo wa anayeshinda kuchukua kila kitu.
Wiki iliyopita, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar
na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali
Mohammed Shein akizungumza na mabalozi wa nyumba kumi wa chama chake,
pamoja na mambo mengine aliwaeleza ikiwa hawautaki mfumo wa SUK ni
lazima CCM ishinde kwa kura nyingi zaidi, pia suala la mfumo huo limo
ndani ya Katiba Zanzibar.
Historia ya siasa za Zanzibar
Historia ya siasa Zanzibar inaonyesha kuwa tangu
kufanyika kwa uchaguzi wa kwanza mwaka 1957 hadi mwaka 2010 hakuna chama
cha siasa kilichoweza kupata kura nyingi zaidi na kwamba matokeo ya
chaguzi hizo ni kura kukaribiana.
إرسال تعليق