SAFARI ya miaka 10 ya kukutana na kimondo 67P imezaa matunda
baada ya chombo maalumu kufanikiwa kutua
salama katika mwamba wa kimondo hicho na kuanza kuleta picha za kustaajabisha
dunia.
Kimondo hicho ambacho kipo umbali wa kilomita milioni 500
kutoka duniani kinakuwa kimondo cha kwanza kufanyiwa uchunguzi wa karibu.
Chombo hicho kilichoandaliwa na Shirika la anga za juu la
Ulaya, Philae, kiliachiana na chombo kingine cha anga za juu kilichokuwa
kikipeleka Rosetta kwa saa saba.
Wataalamu
wamesema baada ya msukoksukso wa kutua chombo hicho kwa sasa kipo salama na
kimeanza kutuma poicha mbalimbali zinazohusu kimondo hicho. Hata hiovyo
wataalamu wamesema kwamba kuna shida ya betri zinazotoa uhai kwa chombo hicho.
Imeelezwa kuwa wakati wa kutua
chombo hicho kilitua kiasi ch akilomita moja nje ya eneo ambalo ilitulia
kutokana na mfumo wake wa kudunda.
Imeelezwa kuwa hali ilivyo kwa sasa itakuwa tatizo kubwa betri hizo kupata mwanga wa kutosha kuzifanya ziendelee kutoa uhai wak chombo hicho.
Kikiwa kimeondoka duniani mwaka 2004 kazi kubwa ni kujifunza kimondo hicho kilivyo ili kutoa sura sahihi ya jinsi mfumo wa jua ulivyoanza.
Chombo hicho Philae kiliwasili katika kimondo hicho 67P/Churyumov-Gerasimenko kikibebwa na setelaiti ya Rosetta baada ya safari ya miaka 10 yenye umbali wa kilomita bilioni 6.4.
Baada ya kufanya uchakmbuzi wa haraka wa picha zilizoletwa na Philae, Dk Stephan Ulamec amesema kwamba huenda kipo katika eneo ambalo awali lilikataliwa kuwa eneo la kutua kutokana na uwezekano wa kuwa ndani ya kreta.
Hata hivyo amesema mazingira ya picha hizo inaonesha kwamba chombo kipo ndani ya kreta ndio sababu ya vurugu zilizopo sasa.
Picha zilizoletwa zinaonesha kwamba Philae imejigandamiza katika ukuta mgumu wa aina yake.
Picha nyingine zinaonesha kwamba ni kama ipo katika mteremko.
Aidha imeelezwa moja ya mguu wake haupo ardhini.
Pamoja na maelezo yote hayo mashaka makubwa ya wataalamu ni mwanga wa kuongezea nguvu betri zilizopo ambazo zinaisha nguvu jumamkosi wiki hii.
Philae inapigwa na mwanga wa jua kwa saa moja na nusu katika mzunguko wa saa 12 wa kimondo hicho, mazingira ambayo hayatatosheleza kuchaji betri zake wakati nishati iliyokuja nayo kutoka Rosetta itakapomalizika.
Paolo Ferri mkuu wa operesheni wa ESA amesema katika hali ya sasa wanatarajia kuwa katika hali ngumu baada ya Jumamosi ingawa itategemea mambo wanayofanya yanayohitaji nguvu kubwa.
Alisema kama wataituma kazi ngumu itamaliza nishati mapema kuliko muda uliopangwa.
Wataalamu wamesema wanaangalia namna ya kubadili mwelekeo wa chombo hicho ili kiweze kutumia mwanga unaoipiga kwa namna inayofaa sana.
Pia wanataka kutumia sehemu zinazoweza kutembea katika chombo hicho kukiondoa katika upande wa giza.lakini inaonekana hakuna muda wa kutosha kuweza kufanya mchakato wa ubunifu.
Hata hivyo kwa sasa wataalamuw anataka kabla ya nishati hiyo kwisha sehemu kubwa ya kazi iliyokusudiwa iwe imemalizika.
Pamoja na matatizo hayo wataalamuw amefurahishwa sana na uwezo wa chombo hicho pamoja na kusafiri kwa miaka kumi.
Hata hivyo walikuwa wanapenda kuchimba udongo ili kuufanyia uchambuzi. Uchimbaji wa udongo huo ndio kisa hasa cha kurushwa kw a chombo hicho.hata hivyo wataalamu wamesema kwamba hawawezi kufanya hivyo kw akuzingatia hali iliyopo kwa hiyo wanasubiri mpaka kazi za kawaida zimalizike ndio wajaribu kwani huenda ndio wakailetea shida zaidi hasa kwa ufukuaji wake.
Pamoja na vikwazo hivyo na chochote kitakachotokea baada ya Jumamosi ni dhahiri kwamba binadamu tayari amejikusanyia taarifa za kutosha kuzifanyia kazi.

إرسال تعليق