![](http://www.itv.co.tz/media/image/msikihela.jpg)
Watu
wasita wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa wilayani Songea
mkoani ruvuma baada ya kupigwa na radi Kufuati mvua kubwa iliyonyesha
usiku huo.
Kamanda
wa polisi wa mkoa wa ruvuma ACP Mihayo Msikhela amesema kuwa Maafa hayo
yalitokea majira ya saa mbili usiku wakati watu hao
Wakila
chakula cha usiku kwenye mgahawa wa chuo cha kilimo na mifugo Cha liti
madaba songea na kwamba mvua kubwa ilinyesha majira ya saa
Moja na nusu hadi saa mbili na baadaye ikapiga radi na kuua watu sita Na kujeruhi watu wawili.
Amewataja
walipopoteza maisha kwa kupigwa na radi kuwa ni Chesco Luoga mwanafunzi
wa chuo cha liti madaba na mkazi wa Ludewa,Lucas
Mabula
mwanafunzi wa chuo hicho na mkazi wa magu mkoani mwanza,Eva
Chapile,muhudumu wa mgahawa wa chuo hicho,Osiana Antoni mhudumu wa
Mgahawa wa chuo hicho,Justine Ngonyani mkulima na mkazi wa madaba Songea na Edwini Fungo mkulima na mkazi wa madaba songea.
Amewataja
majeruhi kuwa ni Beatrice Mhagama mwanafunzi wa chuo cha Kilimo na
mifugo liti madaba na mkazi wa peramiho songea na Leokadia
Fusi muhudumu wa mgahawa wa chuo hicho na kwamba miili ya marehemu na majeruhi wako katika kituo cha afya madaba.
Kutokana
na tukio hilo mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Mwambungu na Mkuu wa
wilaya ya songea Bw.Joseph Mkiriki wameenda eneo la tukio
Madaba songea na kueleza kusikitishwa na tukio hilo na kusema huo ni msiba mzito kwa mkoa wa Ruvuma
- ITV
إرسال تعليق