Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kuna haja ya kubadilisha taratibu za ajira badala ya kuwa za kudumu ziwe za mikataba kwani itasaidia kufanya kazi kwa ufanisi.

Wananchi wa Liwale wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Liwale
mkoani Lindi ambapo aliwaambia kuwa wapinzani kwenye mikoa hiyo hawajai
hata kiganjani hivyo wananchi wasipoteze muda kwa wapinzani.

Vijana
hawakuwa nyuma kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana uliofanyika kwenye uwanja wa michezo Liwale mkoani Lindi.

Wananchi
wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi wakimsikiliza kwa makini Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alipokuwa akihutubia wananchi hao kwenye
uwanja michezo wa wilaya.

Mbunge wa Jimbo la Liwale (CCM) Faith Mitambo akihutubia wananchi wa Liwale kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya michezo vya wilaya ambapo alitoa taarifa za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman akishiriki uvunaji wa korosho wilayani Liwale mkoa wa Lindi.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchanganya zege wakati wa ujenzi wa sehemu za kuchotea maji katika kijiji cha Mpigamiti wilayani Liwale mkoa wa Lindi.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua maji kama ishara ya kuzindua huduma za maji kwa wakazi wa kijiji cha Mpigamiti, mradi huo utahudumia vijiji vingine viwili vya Namakololo na Mitawa ambapo wakazi zaidi ya 6000 watafaidika na mradi huo.

Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Bi.Hadija
Sheweji mkazi wa kijiji cha Mpigamiti mara baada ya kukagua mradi wa
maji.

Katibu
mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM
kata ya Mangirikiti wilayani Liwale mkoa wa Lindi.

Wananchi
wa kata ya Mangirikiti wakifurahia ushiriki wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana kwenye ujenzi wa ofisi ya chama ya kata ya
Mangirikiti ,wilayani Liwale mkoa wa Lindi.
Post a Comment