Stori: Andrew Carlos DEREVA bodaboda mmoja aliyefahamika kwa jina la Seleman amedaiwa kumchoma visu mwilini dereva mwenzake wa aliyefahamika kwa jina la Panya Road na kumsababishia kifo.
![](http://api.ning.com:80/files/Ktsylelmf0kbQv3fYKxFhgxpcmp3cirpfsnaLx45AH2mvzGfnX868tErITkoIEIOBNM2BcmtuAx9vRqNluxy-PahLgR9HRNw/IMG20141210WA0005.jpg)
Dereva
bodaboda anayefahamika kwa jina la Seleman (mwenye flana) akimshambulia
kwa visu mwilini dereva mwenzake anayefahamika kwa jina la Panya Road.
Kwa mujibu wa chanzo, tukio hilo la kusikitisha lilitokea Jumatano
iliyopita asubuhi maeneo ya Tungi-Msikitini, Kigamboni, jijini Dar
katika chumba ambacho Seleman alikuwa amepanga.“Inasemekana Panya Road
ilikuwa kama tabia yake iliyozoeleka ya kumnyatia mwenzake akiwa katoka
kidogo anaingia na kuondoka na chochote cha thamani atakachokikuta.Bahati mbaya leo (Jumatano) Seleman alikuwa ametoka mara moja na mlango wake hakuwa ameufunga sasa aliporudi ndiyo akamkuta Panya Road akiwa ndani kwake akitaka kumuibia ndipo kasheshe lilipoanzia hapo,” kilisema chanzo.
![](http://api.ning.com:80/files/Ktsylelmf0lGoVEC0aK3Upy1mXDgMYHeqNiqMMzERXrqz286LQCA*K2yHivSjysFk2I9rj7JEk2EtdKZIXP4ZusI2eSHJEbS/IMG20141210WA00061.jpg?width=650)
Damu nje nje...
Chanzo kiliendelea kutiririka kuwa baada ya Seleman kumkuta Panya
Road ndani kwake, inadaiwa aliamua kuchukua sheria mkononi ambapo
alichukua kisu na kuanza kumchomachoma sehemu mbalimbali za mwili na
kusababisha avuje damu nyingi.“Tulisikia kelele katika chumba cha Seleman lakini kila tukipiga hodi mlango haukufunguliwa zaidi ya kelele kuongezeka. Hatukukata tamaa tuliendelea kuita mpaka Seleman akafungua mlango lakini nguo zake zilikuwa zimeloa damu,” kilisema chanzo.
![](http://api.ning.com:80/files/Ktsylelmf0k8q*utymn5lvtpuuG*DZbcZRg0unI1MhClJk*VDBnR9PRhIjKTjaIriaqhJ6dLvfSezzHN65vVyH09Q880ODEg/IMG20141210WA0007.jpg)
Raia wakishuhudia tukio hilo.
Baada ya kutolewa nje Seleman, majirani waliendelea kumsihi
asiendelee kumchoma mwenzake lakini hakuacha, alizidisha hadi pale
walipomvaa na kumpora kisu.Hata hivyo baadaye polisi wa Kituo cha
Kigamboni walipigiwa simu na kufika mara moja ambapo walimchukua Seleman
na Panya Road akiwa hajitambui ambapo imedaiwa kuwa alikata roho kabla
hajafikishwa hospitali.Alipotafutwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Kihenya M. Kihenya kuhusiana na tukio hilo, alisema taarifa za tukio hilo hazijamfikia lakini akaahidi kulifuatilia mara moja.
إرسال تعليق