SARA MVUNGI: NINA MIAKA KUMI SIJAFANYA ZINAA

MSANII wa filamu aliyejikita kumtumikia    Bwana kwa nyimbo za Injili, Sara Mvungi amesema kuwa, amechoshwa na upweke wa muda mrefu kwa kuishi bila mwanaume kwa takriban miaka 10 kwa kuwa anasubiri Mungu amshushie mume mwema.
Msanii wa filamu aliyejikita kumtumikia Bwana kwa nyimbo za Injili, Sara Mvungi.
Akitoa la rohoni kwa paparazi wetu, Sara alisema hajajihusisha na masuala ya mapenzi kwa kuwa wanaume wengi wanaomfuata hawaamini, wengi wao ni waongo hivyo anatamani Mungu amshushie chaguo stahiki litakaloufariji mtima wake.
“Ni kipindi kirefu sasa, tangu mwaka 2004 naishi bila mwanaume wala kufanya starehe ya mwili na kama unavyojua suala la zinaa bila ya kuwa kwenye ndoa halimpendezi Mungu na haliendani kabisa na ulokole nilionao, natamani sana kuolewa hata leo lakini sijamuona mkweli katika wote wanaonifuata,”  alisema Sara.

Post a Comment

أحدث أقدم