Breaking News!! MUME AUA MKE KWA KUMPIGA MAKONDE KISA KWANINI AMECHAGUA MGOMBEA WA CCM HUKO TINDE

Habari tulizozipata hivi punde katika chumba cha habari  kutoka katika mtaa wa Mwandu kata ya Tinde katika wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga ni kwamba mwanamme mmoja ambaye jina lake halijajulikana mara moja amemuua mke wake kwa kumchapa makonde kutokana na kile kinachoelezwa kuwa kwanini amechagua mgombea wa CCM badala ya mgombea wa Chadema katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika nchi nzima leo.

Inaelezwa kuwa Jamaa ni mfuasi wa Chadema huku mke wake alikuwa  mfuasi wa CCM.

Tukio limetokea jioni ya leo baada ya mume kumuuliza mkewe kampigia mgombea wa chama kipi leo,mke aliposema CCM ndipo mme akaanza kumpa kipigo hadi mauti kumfika.
Mdau  aliyeko eneo la tukio Paul De Nyoso Seseja anasema kuna taarifa kuwa jamaa alikuwa amebugia pombe na mpaka sasa yuko kwenye mikono ya dola.

Post a Comment

أحدث أقدم