Mwanamke adai kupigishwa mzigo kwa wanaume 200

MWANAMKE mmoja nchini uingereza amedai kuwa amepoigishwa mzigo na wanaume 200 tanguj alipokuwa na umri wa miaka 14 katika kile ambacho polisi wanasema ni utumwa wa ngono.

Mwanamke huyo kutoka Shropshire, ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kwamba mauzo ya  ngono ya lazima yanawezeshwa katika maeneo ya Stratford Road na Ladypool Road yaliyopo Birmingham.

Polisi wamesema kwamba wachunguza kadhia hiyo lakini mwanamke huyo amesema kwamba anataka kuwasaidia wanawke wenzake wasiingie katika mitego hiyo

Polisi  huko West Midlands wamesema kwamba wanawapa elimu watu 1,200 kusaidia kukabiliana na tatizo hilo la soko la ngono.

Awali Halmashauri ya Birmingham ilisema kuna watoto 132 ambao ama wako katika utumwa wa ngono au wanadhulumiwa kwa kufanyishwa biashara ya ngono.

Mwanamke huyo ambaye hakutaka kutambuliwa aliongeza kwamba alikuwa anapelekwa  kufanyishwa ngono katika maeneo yaShropshire na West Midlands.

Alisema alikuwa anakutana na madalali hao kupitia makundi ya vija na wanaojumuika pamoja ambao walikuwa wanampeleka katika maeneo ya migahawa kukutana na wateja wao na kujadiliana malipo.

Alisema wanaume ambao alilala nao walikuwa ni watu wazima na kwamba anakumbuka mmoja alikuwa na umria miaka 80 na kama alikuwa anakataa kutoa huduma alikuwa anapigwa na vyuma au mikanda.

 Alisema wakati fulani alipelekwa na rafiki yake katika mgahawa mmoja ambapo wanaume waliunga foleni kuwachagua yeye au rafiki yake.

"Ilikuwa kama mlango unaozunguka.mmoja baada ya mwingine"alisema.

Post a Comment

أحدث أقدم