![Mapambano Sudan Kusini](http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/304/amz/worldservice/live/assets/images/2014/11/06/141106162441_south_sudan_304x171_ap_nocredit.jpg)
Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu, ICRC, limeonya kuwa mwaka
mmoja baada ya ghasia kuzuka Sudan Kusini mapambano bado yanaendelea
baina ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji na kuhatarisha raia.
Mkuu
wa ICRC nchini humo, Franz Rauchenstein, alisema ingawa waandishi wa
habari wameipa mgongo Sudan Kusini, wale walionasa katika vita hivyo
haifai kuwasahau.Mapigano yalizuka Disemba mwaka jana baina ya wanajeshi wa Rais Salva Kiir na wale watiifu kwa makamo wake wa rais wa zamani, Riek Machar.
Watu kama milioni moja na nusu wamepoteza makaazi na mashirika ya misaada yanasema msaada wa kimataifa unahitajika kuepusha upungufu mkubwa wa chakula.
- bbc
إرسال تعليق