DIAMOND: WEMA, JOKATE, PENNY WALIGOMA KUNIZALIA




KWA mara ya kwanza ndani ya Global TV Online ya Global Publishers, supastaa ndani na nje ya Bongo kutoka muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewafungukia waliowahi kuwa wapenzi wake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, Wema Sepetu ‘Madam’ na Penniel Mungilwa ‘Penny’ kuwa waligoma kumzalia mtoto.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' akiwa katika pozi ndani ya studio za Global TV Online.
LIVE CHUMBA CHA HABARI Akizungumza na Kipindi cha Live Chumba cha Habari kinachorushwa na runinga hiyo kilichofanyika Bamaga-Mwenge jijini Dar, Jumanne wiki hii, Diamond alisema hayo alipoulizwa na waandishi wetu kwamba amekuwa akitangaza kupenda watoto lakini kwa nini hana hata wa dawa licha ya kuwa na uhusiano  na wanawake tofoutitofauti.
Diamond: “Ni kweli napenda watoto lakini siwezi kupata mtoto peke yangu bila mwenzangu. Lazima kuwe na mwenzangu ambaye tutakubaliana.“Nilichojifunza ni kwamba wenzangu hawakuwa real (hawakumaanisha) hivyo wakawa wanachengachenga.”
Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz'akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Penniel Mungilwa ‘Penny’.
PENNY NI ZAIDI YA WOTE Diamond alieleza kwamba, kati ya wanawake aliokuwa nao, Penny ambaye ni mtangazaji wa Radio E-FM ndiye msichana ambaye alikuwa wa kipekee kwani hakuwahi kumkera hata siku moja. “Nimeishi na Penny kwa muda mrefu. Kweli hakunikosea. Sema basi tu.”

MIMBA MBILI KWA PENNY
 “Ukweli Penny ningezaa naye, aliwahi kuniambia ana mimba yangu, sikuamini, nikampeleka hospitali kupima ikawa kweli. Kesho yake niikamnunulia gari, nikamwambia mama tulia. Siku mbili tatu akasema mimba imetoka.

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' akiwa na Wema Sepetu.
“Nikaja nikamjaza kingine cha pili (mimba), nayo baada ya muda akaja kuniambia imetoka. Nikaona huyu mzinguaji, nikammwaga. Lakini iliniuma sana.“Kwa wengine (Jokate na Wema) walikuwa wakinichenga tu bila sababu, unamuona huyu hataki kubeba mimba yangu. Mtu kwa mdomo anasema kwamba yuko na wewe kikamilifu lakini kwa matendo unaona siye.
“Lakini kusema ukweli kabisa natamani sana kuwa na mtoto. “Hapo juzikati nilitaka kuoa, kila kitu kilikuwa sawa, nikaja kubadili mawazo.” Swali: ”Ulitaka kumuoa nani?”Diamond: “Ah! Siwezi kumsema hapa.”
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’
WEMA ALITOA MIMBA YAKE? Alipoulizwa juu ya Wema kama aliwahi kutoa ujauzito wake, Diamond alijibu huku akiachia tabasamu la kiaina:“Siwezi kumsemea yeye labda mumuulize mwenyewe, najua mna mawasiliano mazuri.”
ATAKAMUA DAR LIVE Pamoja na mazungumzo hayo, Diamond ameweka bayana kuwa amejiandaa vilivyo kukamua bonge la shoo la kufunga mwaka, Desemba 25, mwaka huu (X-Mass) kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakheem jijini Dar.

(CHANZO: AMANI/GPL)

Post a Comment

أحدث أقدم