
Siku
zote movie ambayo inasisimua kila sekunde wakati inapotazamwa ndio
movie ambayo huwa mwishoni inasifiwa ambapo kitu kingine kitachofanya
movie iwe bora ni mtazamaji kutojua kitachofata mbeleni wakati
akiendelea kuitazama.
Movie mpya iitwayo Reclaim inazo hizi sifa, ni movie ambayo hata stori yake iliandaliwa kiubunifu sana pamoja na location ilikotengenezewa…. ikiwahusisha Steven na Shannon ambao
walisafiri nje ya nchi na kwenda kununua mtoto ambae waliamua kum-adopt
lakini hawakuwa wanaijua siri kubwa iliyokua nyuma ya Wakala
waliemtumia kumpata huyo mtoto.
Ukiisoma unaweza kuona ni stori ya kawaida ila kiukweli wameitendea
haki kwenye kuitengeneza movie yenyewe, unaweza kuanza na hii Trailer
yake hapa chini.
إرسال تعليق