BAADA ya kusambaa kwa picha nyingi mtandaoni
zikimuonesha akiwa na staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Simwinga ‘Izzo
Business’, mwigizaji Kajala Masanja ameibuka na kueleza kuwa ukaribu huo
ni wa kikazi zaidi.
Staa wa mwigizaji Bongo Movies, Kajala Masanja.
Mapema wiki hii, kupitia mtandao wa
Instagram, Kajala alitupia picha tofautitofauti wakiwa sehemu moja na
Izzo kiasi cha kuzua mashaka ndipo mwandishi wetu alipoingia mzigoni na
kumuuliza Kajala kulikoni? Huyu hapa msikie:
Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Simwinga ‘Izzo Business akipozi.
“Kuna project tunataka kufanya ndiyo maana unaona nimekuwa naye
karibu kwa muda mrefu na mapichapicha ya selfie tukapiga, hakuna zaidi
ya kazi ya filamu ninayotaka kufanya naye.”
إرسال تعليق