MTOTO mzuri Bongo Movies, Rose Ndauka amewatega
mashabiki wake kwa kutupia picha ya kidole chake chenye pete ya uchumba
kwenye mtandao wa Instagram kuashiria kuwa amechumbiwa.
Mtoto mzuri Bongo Movies, Rose Ndauka.
Mara baada ya paparazi wetu kuiona picha hiyo iliyozua mjadala mkubwa
mtandaoni, alimtafuta Rose na kumtaka afunguke kama amechumbiwa upya
baada ya kumwagana na aliyekuwa mchumba’ke, Malick Bandawe hivi
karibuni. Msikie alivyojibu:
Kidole cha Rose Ndauka kikiwa na pete ya uchumba.
“Kweli picha ni yangu, mimi ndiye nimeiweka, kuchumbiwa ni jambo la
kheri lakini siwezi kusema kama tayari au bado, muda ukifika
nitawaambia.”
إرسال تعليق