Na Lorietha Laurence - MAELEZO
Serikali
imejidhatiti katika kuboresha huduma za mawasilano kwa Njia ya Mtandao
(TEHAMA) ili kurahisisha utendaji wa shughuli mbalimbali za
kiserikali.
Akiongea
na wajumbe wa bodi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA),
jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema
lengo la Serikali ni kuongeza ufanisi kwa watumishi na jamii kwa ujumla
kujifunza na kuwasilisha mada mbalimbali kupitia mtandao.
Balozi
Sefua amesema kuwa serikali na taasisi zake mbalimbali hazina budi
kutumia wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao kufanya shughuli zake zote
zinazotekelezeka kwa njia ya Videoconference na Mafunzo ya Masafa ili
kupunguza gharama.
“Lengo
kuu la Serikali ni kurahisisha mawasilino baina ya watumishi na jamii
ili kupunguza usumbufu wa safari ndefu kutoka sehemu moja kwenda
nyingine na pia kuokoa muda, na urahisi wa upatikanaji wa huduma kwa
wananchi” alisema.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao
(TaGLA), Bwana Charles Sekondo, amesema ofisi yake imekuwa ikitekeleza
majukumu kwa ufanisi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
wanaojihusisha na mafunzo kwa njia ya mtandao ili kwenda sambamba na
maendeleo ya teknolojia duniani katika utekelezaji wa shughuli
mbalimbali za kijamii na kiserikali.
“Wakala
wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao imerahisisha sana mawasiliano baina ya
serikali, wizara, idara , wakala wa Serikali, pamoja na Sekta binafsi
katika kuboresha uweledi kiutendaji kupitia utawala bora, anuai za
jamii, maswala ya afya na mazingira” alisema Sekondo.
Katika
Ziara hiyo Katibu Mkuu Kiongozi alitembelea maeneo mbalimbali ya ofisi
ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao ikiwemo Sehumu ya Huduma za
Video Conference, Chumba cha Maabara za Kompyuta na kituo cha taarifa za
maendeleo (TDCI).
Mtandao
wa TaGLA unajukumu la kuwajengea uwezo watumishi wa wizara, idara na
wakala wa serikali pamoja na sekta binafsi katika nyanja mbalimbali
ikiwemo , mafunzo ya midahalo kwa njia ya video ya hapa nchini na nchi
nyingine, midahalo kwa njia ya mtandao, mafunzo ya ana kwa ana na
mafunzo kwa njia ya uongozi.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wanne Kushoto)
akifuatilia kwa umakini mazungumzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya,
alipotembelea ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa),leo jijini
Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wanne Kushoto)
akifuatilia kwa umakini mazungumzo kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya,
alipotembelea ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa),leo jijini
Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wanne Kulia) akitoa neno
la shukrani kwa watu wa Kenya baada ya mazungumzo kwa njia ya mtandao , alipotembelea
ofisi ya Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLa),leo jijini Dar es Salaam,
kulia kwake ni Mkuu wa Chuo cha IFM Pro. Daniel Mjema, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bwana George
Yembesi na Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA, Bwana Charles Senkondo.
Wajumbe wa bodi ya Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya
Mtandao(TaGLa) wakifuatilia mazungunzo
kwa njia ya mtandao na watu wa Kenya, Mafunzo kwa njia ya mtandao
(TaGLa),leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa tatu kushoto)
akifurahia jambo baada ya kupata maelekezo namna mitambo ya mawasiliano
inavyofanya kazi kutoka kwa Menaja wa tecknolojia TaGLA ,Bwana Emmanuel Tessua
wa kwanza kushoto,na Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA ,Bwana Charles
Senkondo(katikati) leo jijini Dar es Salaam.
Menaja wa tecknolojia TaGLA ,Bwana Emmanuel Tessua
wa kwanza kushoto, akitoa maelekezo kwa Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa
pili kulia) ya namana mikutano inavyofanyika kwa kutumia mtandao katika
chumba cha mikutano wakati wa Ziara yake leo jijini dare s Salaam
, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Bwana
Charles Senkondo leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (katikati) akitembele ofisi za Wakala wa Mafunzo
kwa njia ya mtandao (TaGLa) katika ziara yake leo jijini Dare s Salaam, mbele
ni Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA, Bwana
Charles Senkondo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Bwana Charles
Senkondo akitoa maelekezo kwa Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika
kituo cha taarifa za maendeleo(TDIC) alipotembelea ofisi hizo leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Bwana Charles
Senkondo akitoa maelekezo kwa Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika
kituo cha taarifa za maendeleo(TDIC) alipotembelea ofisi hizo leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ( wa tatu kushoto) akiangalia namna majadiliano yanavyofanyika
kwa mfumo wa kutumia mtandao katika
ofisi za Wakala wa Mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLa) wakati wa ziara yake leo
jijini Dare s Salaam, wa kwanza kushoto ni Menaja wa tecknolojia TaGLA ,Bwana
Emmanuel Tessua na wa pili ni Mkurugenzi
Mtendaji wa TaGLA Bwana Charles Senkondo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa kwanza kulia) akiangalia moja ya vitabu vinavyohifadhiwa
katika kituo cha taarifa za maendeleo kilichopo katika ofisi za Wakala wa
Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara
yake katika ofisi hizo , kushoto kwake
ni Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA, Bwana Charles Senkondo na wengine ni wajumbe
wa bodi ya TaGLA.
Picha na Lorietha Laurence- MAELAZO
إرسال تعليق