Kikosi cha Rais chafanya jaribio la mapinduzi

KIKOSI cha Ulinzi wa rais nchini Gambia kimeasi na kufanya jaribio la mapinduzi  wakati rais wa taifa hilo yupo Ughaibuni.
Imeelezwa kuwa milio ya risasi ilisikika karibu na kasiri la Rais Yahya Jammeh, mjini Banjul.
Ingawa habari zilizopatikana  ni za hado hado,duru za kijeshi na za kibalozi zimesema kwamba kikosi cha ulinzi wa rais kilikuwa kilifanya jaribio la mapinduzi.
Jammeh mwenyewe alichukua mamlaka baada ya kufanya mapinduzi na sasa analaumiwa kwa utawala wake unaodaiwa kukandamiza wananchi na upinzani.
Hata hivyo imeelezwa katika duru za kijeshi kwamba kikosi hicho kimesambaratishwa na wanajeshi watiifu.
Hakuna taarifa rasmi kiongozi huyo yuipo wapi . Baadhi ya vyombo vya habari vinasema yupo Ufaransa na vingine vinasema yupo Dubai.
Katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) mwaka 2011, Jammeh alisma kwamba atatawala Gambia kwa miaka bilioni .
Taifa hilo ambalo fukwe zake zina mchanga wa kupendeza ni maarufu sana kwa utalii.

Post a Comment

أحدث أقدم