Zifahamu talaka 5 aghali zaidi za mastaa wa Hollywood

Wakati ambapo Chris Rock na mke wake wa zaidi ya miaka 18, Malaak Compton-Rock wakipeana talaka, mtandao wa Page Six umetoa orodha ya talaka tano zilizogharimu fedha nyingi zaidi. Nazo ni:
Mel Gibson na Robyn Moore


Mastaa hawa walioana kwwa kipindi cha miaka 28 kabla ya kuamua kuachana. Baada ya talaka yao kuwasilishwa, Robyn alipewa nusu ya dola milioni 850 za Mel na kufanya kuwa talaka aghali zaidi kwenye historia. Walikuwa na watoto saba pamoja.
Michael na Juanita Jordan



Kwa mujibu wa Forbes, Juanita aliyeolewa na mcheza kikapu wa zamani wa NBA, Michael Jordan mwaka 1989 na kupata watoto watatu, alipewa dola milioni 168 kwenye talaka yao mwaka 2006.
Neil Diamond na Marcia Murphey
Neil and Marcia Diamond
Neil ambaye ni muimbaji aliolewa na Murphey, mtayarishaji wa TV mwaka 1969, na walipata watoto wawili pamoja kabla ya kuachana 1995. Diamond alipewa dola milioni 150 kutokana na talaka.
Tiger Woods na Elin Nordegren

File photo of Tiger Woods and Elin Nordegren at an NBA basketball game in Orlando
Mchezaji huyo wa golf na mke wake Msweden aliyekuwa yaya kabla ya hapo, waliachana mwaka 2009. Wawili hawa walizaa watoto wawili. Nordegren alilipwa dola milioni 100.
Steven Spielberg na Amy Irving
Ron Galella, Ltd.
Mwaka 1989, baada ya miaka minne ya ndoa, muongozaji huyo wa filamu kama “Jaws” na “E.T.,” na mke wake muigizaji waliachana. Mke wake alilipwa dola milioni 100.

Post a Comment

أحدث أقدم