Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa
Mtwara mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa
Mashujaa ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kazi ya CCM ni kuisimamia
Serikali kutimiza wajibu wake kwa wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa mkoa
wa Mtwara ambapo aliwaambia matatizo yao sugu ya korosho, bandari na
kukatika kwa umeme lazima yapatiwe ufumbuzi kwa kutaka Mawaziri wa
wizara husika kuja na majibu .
Wananchi wa Mtwara mjini wakishangilia kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa mgeni rasmi akiwa Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Umati wa wakazi wa Mtwara wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye alipokuwa anahutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye viwanja vya Mashujaa ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa Chama
Cha Mapinduzi ni chama chenye kufuata Kanuni na Taratibu na wale wote
ambao watakiuka utaratibu hawana budi kuachia ngazi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mtwara
mjini ambapo aliwaambia wapinzani wengi wamekosa sera za msingi na
badala yake wanafanya shughuli za kiharakati na si siasa.
Wananchi wa Mtwara wakishangilia kila neno kutoka kwa viongozi wao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisisitiza kwa wananchi hao kuwa
wanaipa kura ya ndio CCM kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa
utakaofanyika Desemba 14 mwaka huu.
Mbunge wa Mtwara Mjini Ndugu Hasnain Murji akieleza utekelezaji wa
ilani ya CCM ulivyotekelezwa vizuri kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa ambapo pia alieleza changamoto
zinazowakabili wananchi wa Mtwara mjini hivyo kumtaka Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana kusaidia katika kufanikisha baadhi ya mambo
ambayo yameonekana kukwamishwa na viongozi wa juu serikalini.
Wananchi
wakizunguka gari la Katibu Mkuu wa CCM baada ya mkutano kumalizika
kwenye viwanja vya Mashujaa jana tarehe 30 Novemba 2014.
إرسال تعليق