
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa mjini
Mtwara katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya
Mashujaa mjini humo akihitimisha ziara yake ya siku 16 aliyoifanya
katika mikoa ya Lindi na Mtwara akikagua utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali kwa
kushirikiana na wananchi wenyewe na kuhimiza uhai wa chama cha Mapinduzi
CCM.
Katika
ziara hiyo Katibu mkuu huyo aliongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC
Itikadi, Siasa na Uenezi, Katika kutano huo Kinana amempa wiki mbili
Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe kutoa maelezo kwanini bidhaa
mbalimbali hazisafirishwi kwenda nje kupitia bandari ya Mtwara, Lakini
pia Kinana amewaagiza Waziri wa Nishati na Madini kutoa maelezo ni
kwanini wawekezaji wenye kampuni zinazofanya shughuli zao mtwara
wanalipia kodi zao jijini Dar es salaam badala ya kulipia mkoani Mtwara
ambako wanafanya shughuli zao.
Pia
waziri wa Ofisi ya Mkamu wa Rais Mazingira amepewa mwezi mmoja
kuhakikisha dampo la taka za sumu zinazotupwa na wachimbaji wa gesi na
viwanda kuacha mara moja kwa sababu zinahatarisha maisha ya wakazi wa
Mtwara, Mwisho akaagiza Ofisi ya Waziri Mkuu kutoa kibali cha kugawa
viwanja katika manispaa ya Mtwara kwani viwanja vimeshapimwa, Fedha za
kulipa fidia zipo ila kibali kutoka ofisi ya Waziri mkuu ndiyo kimkwama
kwa muda wa mwaka mmoja sasa.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA
FULLSHANGWE-MTWARA).

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati
alipokuwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara.

Wananchi
wakinyoosha mikono yao juu kufurahia hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akiwahutubia.

Mbunge
wa jimbo la Mtwara mjini Mh. Hasnein Murji akiwahutubia wapiga kura
wake ambao walifurahia sana hotuba yake kwenye viwanja vya Mashujaa
mjini Mtwara.

Umati wa wananchi ukiwa umefurika katika mkutano huo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi mbalimbali katika meza kuu wakati wa mkutano huo.

Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.

Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape nnauye wakiingia katika uwanja wa mkutano.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangali vikundi vya ngoma mara baada ya kuwasili katika mkutano wa hadhara.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia Nape Nnauye na viongozi wa mkoa wa Mtwara wakiwasili katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia Nape Nnauye na viongozi wa mkoa wa Mtwara wakiwasili katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara.
إرسال تعليق