Stori: Gladness Mallya SIKU
chache kabla ya kupatwa na umauti, mnenguaji mkongwe Bongo, Mwanaisha
Mbegu ‘Aisha Madinda’ alifunguka maneno ambayo yalionesha dhahiri kama
alikiona kifo chake. Kwenye mazungumzo hayo aliyozungumza na mwanahabari
wetu, Aisha alisema atatoa habari nzito ambazo zitaripotiwa na magazeti
matatu na kudai ni ‘sapraiz’.
“Nina furaha sana kwa sababu nimerudi salama kutoka Dubai nilikokuwa nalazimishwa kufanya kazi za ndani nikakataa, ukweli watoto wangu wamefurahi sana kwa sababu nimerudi nikiwa na afya njema.
“Niko fiti nimeachana na madawa ya kulevya sasa hivi nimerudi rasmi kwenye kazi yangu ya unenguaji, nitakutafuta siku nikupe habari kubwa ambayo sijawahi kuzungumza sehemu yoyote yaani itakuwa ni nzuri na utatoa magazeti matatu,” alisema Aisha ambapo Desemba 17, mwaka huu alifariki dunia kabla ya kutimiza ahadi hiyo kwa mwandishi wetu.Aisha aliyeacha watoto wawili wa kiume na wa kike, alitarajiwa kuzikwa jana nyumbani kwake Kigamboni, jijini Dar.
Mnenguaji mkongwe Bongo, Mwanaisha Mbegu ‘Aisha Madinda’.
Licha ya paparazi wetu kumdodosa aseme habari hizo, alikataa na kusema itakuwa ni sapraiz.“Nina furaha sana kwa sababu nimerudi salama kutoka Dubai nilikokuwa nalazimishwa kufanya kazi za ndani nikakataa, ukweli watoto wangu wamefurahi sana kwa sababu nimerudi nikiwa na afya njema.

إرسال تعليق