LULU MAWIGI YANATUZEESHA JAMANI

Stori: Imelda Mtema STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa, mawigi wanayovaa mastaa mbalimbali akiwemo yeye, yanawazeesha sura na kuonekana  wakubwa kupita kiasi kumbe sivyo ilivyo.
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Lulu alisema, mara nyingi mastaa wanapenda kujaza mawigi makubwa kichwani mwao lakini kiukweli wakiondoa mawingi hayo na kusuka hata tano kichwa wataonekana wadogo sana hivyo ni vyema wakabadilika.
“Nilijaribu kuweka mawigi pembeni na kujisukia tano kichwa changu kwa kweli naonekana katoto kabisa hapo ndipo nilipogundua kuwa mawigi kwa kipindi kingine siyo kabisa yanatuzeesha tu,” alisema Lulu.

Post a Comment

أحدث أقدم