Mapenzi yake yalizidi kwa mbwa, akaomba azikwe nae baada ya kufariki…

20110425_German_Shepherd_Dog_8505
Kutokana na mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwa mbwa wake huyo, huenda aliona kama iwapo atatangulia kufariki mbwa wake hatopata upendo kama anaompatia yeye.
Akiwa hai aliomba kama ikitokea yeye akafariki kabla ya mbwa wake basi wazikwe pamoja.
Mwanamke huyo Connie Lay raia wa Indiana, Marekani aliyefariki siku chache zilizopita aliacha ombi hilo kwa rafiki zake, atakapokufa yeye na mbwa wake wazikwe pamoja, baada ya kufariki marafiki hao walituma ombi hilo kwa maafisa wanaoshughulikia haki za wanyama ambaowalipinga ombi hilo.
Mbwa huyo aliyepewa jina la Bella, Lay alitaka azikwe naye ambapo ombi hilo lilipingwa na watu wa haki za wanyama huku wengine wakitaka kujitolea kumlea mbwa huyo ili aepukane na adhabu hiyo ya kifo.

Post a Comment

أحدث أقدم