‘Mkataba Sserunkuma umeghushiwa saini’

http://www.futaa.com//images/350x300/962662542sserunkuma.jpg 
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Express ya Uganda, Francis Ntalazi amedai Simba ilitumia saini ya kughushi kupata mkataba wa Simon Sserunkuma kama mchezaji huru.
Ntalazi alilalamikia kitendo cha kughushi saini yake katika mkataba wa mchezaji huyo kilichofanywa na mmoja wa viongozi wa klabu hiyo.
“Ilinishangaza kwani hakuna mtu anayeruhusiwa kusaini  badala ya mtu mwingine bila idhini ya mhusika, ninapeleka suala hili polisi na tayari nimeshawaelekeza mawakili wangu kufuatilia jambo hilo,” alisema Ntalazi.
Pia, ameishauri Simba iende Uganda kuwasiliana na kufanya mazungumzo halali kama wanamtaka mchezaji huyo kwani kwa mpango waliofanya wamemchukua bure na kwa saini ya kughushi.
“Lakini sishangazwi na baadhi ya watu waliokuwa wanajua jinsi mkataba ilivyokuwa, ninachotaka ni Shirikisho la Soka Uganda (Fufa) kuingilia kati na haki itendeke,” alisema.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspoppe alisema tayari Sserunkuma amepata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) na wanategemea atarejea wakati wowote na kujiunga na wenzake kwa ajili ya kujiandaa na ligi.
“Hatujasikia pingamizi lolote kutoka kwa uongozi wa Express, mchezaji tumemsajili na alirudi Uganda kufuata ITC ambayo tayari ameshaipata,” alisema.
Kwa mujibu wa kanuni za ITC, hakuna mchezaji anayeruhusiwa kuifuata mwenyewe kwa sababu uhamisho hufanywa kieletroniki na kuhusisha mashirikisho.
Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura alisema bado hawajapokea ITC ya Simon Sserunkuma

Post a Comment

أحدث أقدم