Kamanda wa Umoja wa Vijana
wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Iringa Mjini, Frederick Mwakalebela
ametoa tena zaidi ya Sh Milioni 14 kudhamini ligi ya soka ngazi ya wilaya,
Iringa Mjini.
Hiini mara ya pili kwa
mdau huyo wa soka aliyewahi pia kuwa Katibu wa Shirikishola Soka Tanzania (TFF)
kuidhamini ligi hiyo ambayo kabla yake ilikuwa ikichezwa bila washindi kupata
zawadi yoyote ile.
KatibuMsaidizi wa Chama
cha Soka Iringa Mjini (IMFA), Rashid Shungu alisema katika hafla fupi ya
uzinduzi wa ligi hiyo mjini hapa jana kwamba: “baada ya Mwakalebela kujitokeza
kudhamini ligi hii, timu zote zinapata vifaa vyamichezo, mashindi wa kwanza
hadi wa tatu wanapata zawadi na waamuzi na viongoziwanaosimamia ligi hiyo
wanapata posho.
Alisemakwa kupitia
udhamini huo, mshindi wa kwanza anapata kikombe, Sh 500,000 namipira mitano,
mshindi wa pili anapata sh 300,000 na mipira mitatu na mshinditatu anapata Sh
200,000 na mipira miwili.
Akikabidhi vifaa (jezi na
mipira kwa timu hizo), Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa waIringa (IRFA),
Cyprian Kwihyava aliahidi kumuongezea mshindi wa kwanza wa ligihiyo, Sh 500,000
na hivyo kufanya mshindi atakayepatikana mwaka huu kuondoka najumla ya Sh
Milioni moja.
Kwihyavaalisema wananchi
wa mkoa wa Iringa wana kiu kubwa ya kuona moja au zaidi yatimu zake zinapata
mafanikio katika mchezo huo na kushiriki ligi kuu Tanzaniabara.
Akitoasababu ya kudhamini
ligi hiyo, Mwakalebela alisema: “ligi hii ni moja ya liginyingi za chini
zinazoweza kusaidia kuibua vipaji vinavyoweza kuboresha mchezohuu mjini Iringa.
Alisemaakiwa mmoja wa
wadau wa soka nchini, ameamua kurudi nyumbani Iringa nakushirikiana na wadau
wengine kuinua mchezo huo.
“Pamojana udhamini wangu,
natoa wito kwa wadau wengine wajitokeze kuziunga mkono timuzetu ili malengo
tuliyonayo katika sekta hiyo yaweze kufikiwa,” alisema.
Timu zitakazoshiriki ligi
hiyo ni pamoja na Gangilonga FC, Mkimbizi United, IlalaFC, Feed Force FC,
Miyomboni FC, Mkwawa FC, Black Eagle FC, Iringa Downtown FC,Upendo Shooting
Stars, Black Cheaters FC na Young Boys.
Source:Picha, stori na Frank Leonard,Iringa Press
Post a Comment