Ndugu wa abaria waliopotea kwenye ndege ya AirAsia wakilia kwa uchungu
Hali
mbaya ya hewa imechelewesha zoezi la anga na majini la utafutaji wa
ndege ya AirAsia aliyoanguka ikiwa na watu 162 baada ya kuwepo kwa
dhoruba katika pwani ya eneo la Borneo siku ya jumapili.
Kufuatia
kupatikana kwa vipande vya mabaki ya ndege hiyo siku ya jumannne,
kiongozi wa taasisi ya uokoaji na utafutaji amesema miili mitatu
imepatikana hadi sasa kutoka katika eneo la bahari ya Java.
Wapiga
mbizi wa kikosi cha maji cha jeshi wanatarajiwa kuanza kutafuta miili
na kinasa sauti cha ndege hiyo katika kina cha chini cha maji katika
eneo linalosadikiwa ndipo ndege hiyo ilipoangukia.
Ndege hiyo ilipotea ikiwa safarini ikitokea mji wa Surabaya nchini Indonesia kuelekea nchini Singapore.(BBC)
إرسال تعليق