Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Baraza
la Usalama la Umoja wa mataifa limekataa azimio lililoandaliwa na
Palestina ambalo limewasilishwa na Jordan linalopendekeza kusitishwa kwa
mpango wa Israel wa kuyakalia maeneo ya Palestina kwa miaka miaka
mitatu.
Jordan iliwasilisha azimio hilo baada ya kukubaliwa na nchi 22 za kiarabu ikiwemo mamlaka ya Palestina.
Kura tisa zilihitajika ili kupitisha azimio hilo lakini azimio hilo lilipigiwa kura nane pekee.
Nchi
mbili zilipiga kura ya hapana kupinga azimio hilo ambazo ni Australia
na Marekani zilizokataa mpango huo wa mwisho na kusema hautasaidia
katika masuala ya usalama wa Israel.
Nchi tano hazikupiga kura
ambazo ni Uingereza, Lithuania, Nigeria, Jamuhuri ya Korea na Rwanda,
huku Urusi, China, Ufaransa, Argentina, Chad, Chile, Jordan na
Luxembourg zikilipigia kura ya ndio azimio hilo(BBC)
إرسال تعليق