MSANII wa
filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amezua gumzo baada ya picha zake
zinazomuonesha akiwa chumbani na mwanaume kuenea mtandaoni, huku kijana
huyo akionekana kujichora tatoo yenye jina la mwanadada huyo.
Kijana
huyo aliyefahamika kwa jina moja la Brown hakuweza kupatikana ili
kuthibitisha uhusiano wake na mrembo huyo, lakini Rayuu alikiri kuwa
ingawa picha iliyowekwa mtandaoni ilionyesha wakiwa kikazi zaidi, huyo
ni mpenzi wake wa siku nyingi.
“Hizo
picha ni sehemu ya vipande vya kwenye wimbo wa huyo mwanaume, ukweli ni
mpenzi wangu wa siku nyingi na anataka kunioa, ndiyo maana kafikia
hatua ya kujichora jina langu, sina kipingamizi, tunaomba Mungu
atufanikishe tufunge ndoa,” alisema.



إرسال تعليق