Patcho Mwamba akiwa katika ofisi za Global Publishers Ltd leo.
Picha ya Patcho iliyozua utata mitandaoni.
MWIGIZAJI na mwanamuziki wa Bendi ya FM
Academia, Patcho Mwamba hivi punde ameibuka katika ofisi za mtandao huu
na kukanusha vikali taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa
amefumaniwa akiwa na mke wa mtu na kupokea kipigo.
Akiongea na mtandao huu, Patcho amesema picha iiliyozagaa mitandaoni
aliipost mwenyewe juzi baada ya kupata aleji ya macho ambapo baadaye
ilisambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa kapigwa baada ya fumanizi."Unajua nina aleji na pombe pamoja na vumbi, nikitumia tu pombe lazima macho yangu yavimbe
juzi nilikunywa Windhoek mbili na usiku hali yangu ikabadilika na macho kuvimba, baada ya tukio hilo niliamua kujipiga picha na kuipost katika mtandao wa Instagram na hapo ndipo balaa likazuka" Alisema Patcho akiwa katika ofisi za mtandao huu zilizopo Mwenge-Bamaga, Dar.
Post a Comment