Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa vijana wengi hupoteza maisha
wakiwa na umri mdogo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo kutokuwa na
utaratibu wa kupima afya mara kwa mara ili kubaini magonjwa kabla
hayajakomaa.
Hayo yalisema jana na Katibu wa Umoja wa Vijana wa
Wanakahama, Daud Ng’osha wakati wa kuhamasisha jamii kupima afya mara
kwa mara.
Alisema hivi vijana wengi wamekata tamaa ya kuishi
miaka 50 kutokana na kuandamwa na magonjwa ambayo yangeweza kuzuilika
kama yangegundulika mapema kwa utaratibu wa kupima afya.
“Vijana wanakata tamaa kutokuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara,” alisema.
“Lengo la kuunda umoja huu ni kuikumbusha jamii
kuwa na utaratibu wa kupima afya ili kujitambua na kuishi maisha ya
amani, kwani sasa vijana wengi wamekata tamaa ya kuishi miaka mingi,”
alisema Ng’osha.
Awali, Mwenyekiti wa Wanakahama, Sweetbert Nkuba
aliwahimiza vijana na jamii kujitokeza kwa wingi kupima afya, kwani
magonjwa mengi yanatibika yaligundulika mapema.
Tunapaswa kupima afya ili kubaini matatizo mapema na kuyashughulikia,” alisema Nkuba.
إرسال تعليق