Dar es Salaam. Wagonjwa wa saratani wa mikoani wanatarajiwa
kupata matibabu ya kwa njia ya mtandao baada ya Kampuni ya Simu Tanzania
(TTCL) kuzindua huduma ya afya ya mtandao.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja TTCL, Laibu
Leonard alisema hayo juzi alipokabidhi msaada wa vyakula wa Sh3 milioni
katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Alisema huduma hiyo itamwezesha mgonjwa kupata matibabu akiwa katika moja ya hospitali za rufaa nchini.
Laibu alisema hata tiba ya mionzi itafanyika kwa kushirikisha madaktari bingwa waliounganishwa na huduma hiyo ya kisasa zaidi.
“Hakuna haja ya kwenda India, Uingereza, Ujerumani
au nchi nyingine kwa ajili ya tiba, unaweza kufanyiwa upasuaji Bugando,
Ocean Road, KCMC au Tumbi,” alisema.
Alisema lengo lao ni kuunganisha hospitali zote za rufaa nchini ifikapo Machi mwakani.
- Mwananchi
- Mwananchi
إرسال تعليق