Dar es Salaam. Chama cha Wanasheria Wanawake
(Tawla) kimezindua Ripoti ya Mapitio ya Ukatili wa Kijinsia nchini na
kubaini kukithiri kwa matukio hayo waliyodai yanasababishwa na udhaifu
wa sheria.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo
jijini hapa jana, mwenyekiti wa Tawla, Aisha Bade alisema chama hicho
kilifanya utafiti katika baadhi ya mikoa na wilaya nchini na kubaini
kuwa kuna upungufu mkubwa wa kisheria katika masuala ya unyanyasaji wa
kijinsia.
“Tulienda mbali zaidi na kuangalia ni kwa kiwango gani sheria na sera zinaangalia ukatili wa kijinsia,” alisema Bade.
Kadhalika Bade alisema ripoti yao ilibaini kuwa
masuala mengi ya ukatili wa kijinsia yana mizizi katika usawa na
yanasababishwa na wanajamii wenyewe, tamaduni na mazingira. Ongezeko la
matukio ya ukatili wa kijinsia lilionyeshwa katika utafiti uliofanywa na
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa) mwaka 2013 pekee kesi
190 za ubakaji ziliripotiwa kwenye mikoa ya Singida na Dodoma, pamoja na
wilaya za Babati, Newala na Mbulu huku kesi 996 zikiripotiwa Unguja.
Kuhusu sheria zenye upungufu, Bade alisema sheria
mpya ya ndoa bado haiweki wazi umri sahihi wa kuolewa, jambo
linalosababisha ndoa za utotoni.
Sheria zenye udhaifu zilizoibuliwa na Tawla ni
pamoja na sheria mpya ya mtoto ya mwaka 2009 ambayo haiweki wazi umri wa
kuolewa au kuoa na sheria maalumu ya makosa ya kujamiiiana (Sospa).
إرسال تعليق