MKUU
wa Polisi Wilaya ya Mjini, Ali Makame (wa pili kushoto) akiangalia gari
iliyovunjwa na kuibiwa pesa zinazosadikiwa kuwa ni euro elfu moja na
shilingi za kitanzania milioni tano, muda mfupi baada ya kufika eneo la
tukio katika eneo la Mlandege mjini Zanzibar.
ASKARI
Polisi wakiwa wameizunguka gari iliyovunjwa na kuibiwa pesa
zinazosadikiwa kuwa ni euro elfu moja na shilingi za kitanzania milioni
tano, tukio hilo limetokea majira ya saa saba mchana katika eneo la
Mlandege mjini Zanzibar leo. Mmiliki wa gari hiyo aliegesha gari yake na
kuingia msikitini kwa kusali sala ya Ijumaa katika msikiti jirani na
maengesho ya gari katika eneo la mlandege. (Picha na Haroub Hussein).
إرسال تعليق