Ushoga suala tata haki za binadamu


IMG_6695
Mgeni rasmi Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mh Ali Hassan Rajab akizungumza wakati wa akifungua mkutano wa kujadili utekelezaji wa makubaliano ya haki za binadamu nchini na maandalizi ya ripoti ijayo ulioenda sambamba na maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani.
Wengine meza kuu ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bibi Mary Massay, Mkuu wa Balozi za Umoja  wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Afrika Mashariki Filiberto Ceriani-Sebregondi na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani yaliyoenda sambamba na mkutano wa kujadili utekezaji wa makubaliano ya haki za binadamu na maandalizi ripoti ijayo.
Na Mwandishi wetu
KAMISHNA wa  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ali Hassan Rajab  amesema kwamba suala la haki za mashoga, ni suala tata kwa kuwa ni kinyume cha maumbile na sheria.
Kauli hiyo ameitoa siku ya Haki za binadamu katika mahojiano na waandishi wa habari kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazokabili Tume yake katika kuhakikisha haki za biandamu nchini.
“Sisi tumeumbwa na katika maumbile yetu kila mmoja alipewa haki yake sasa tukiitumia isivyokusudiwa basi tunavunja haki. Tukitumia tunavyokusudia tutakuwa juu ya mstari, “ alisema kamishna huyo na kuongeza kuwa kama kuna watu wanahisi kuwa vile ni haki ajue kwamba anakwenda kinyume na maumbile na sheria.
Kamishina huyo alisema ingawa watu hao wanajivisha joho la haki za binadamu wakisema ni haki zao kuwa mashoga, hiyo si utamaduni.
Hata hivyo alisema kuwa matendo hayo ni sawa na watu kuumbwa na mdomo kwa ajili ya kula chakula lakini mtu akapeleka puani.
Alisema hayo ni maoni yake na kwamba  watu hao wanapaswa kuelewa kuwa maumbile hayaruhusu na  vyema wajue sheria ili waweze kuishi vizuri.
 “Ingawa pengine utahisi kwamba hiyo ni haki yako na unayeifanya unaona haina madhara, baadaye itakuwa na madhara. Madhara yake ni kama UKIMWI na magonjwa ya gono na mengine kwa sababu tu ya kwenda tofauti ya maumbile yanayotakiwa kwenda,” alisema.
Alisema pamoja na ukweli huo katika masuala ya haki za binadamu kuwa kuna changamoto nyingi katika suala hilo la haki za binadamu na utawala bora.
Alisema juhudi zinatakiwa kuelekezwa kwa wananchi kwa sababu ya kuwepo kwa mila nyingi zinazonyima haki.
Akizungumzia mauaji yanayofanywa na  vyombo vya dola, alisema kwamba watu 80 walikufa kati ya mwaka 2006 na 2010 na kwamba sasa wanauliza wahusika sababu ya mauaji hayo.
Alisema ni kazi ya Tume kuhoji matukio,sababu au mazingira ya vifo.
Siku ya haki ya binadamu iliyoanza kusherehekewa mwaka 1948  pia kwenye miaka ya 1990 ilianzisha mfumo wa mapitio wa kipindi maalumu ya nchi kuhusu mpango mkakati wa haki za binadamu.
Mfumo huo wa mapitio katika kipindi maalumu katika kujitathmini na kujipima katika utekelezaji wa haki za binadamu ndio unaangalia yapi ya kutekeleza katika kuhakikisha haki za binadamu zinapatikana siku zote.

Post a Comment

Previous Post Next Post