Wanasiasa wanaosaka urais 2015 waonywa

Jumuiya ya Taasisi ya  Elimu ya Juu nchini  (Tahliso), imewashukia wanasiasa wanaotaka kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao kuacha kuutumia umoja huo kama mtaji wa kisiasa wa kupata nafasi hizo.
Mwenyekiti mpya wa Tahliso, Francico John, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu na uchaguzi alisema wanasiasa hapa nchini hususani wanaotaka kuwania urais katika uchaguzi mkuu mwakani wamekuwa wakiutumia umoja huo na kusababisha kuzuka kwa migogoro.

Alisema kuwa Tahiliso siyo chombo cha kisasa wala dini bali kimeanzishwa kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa vyuo vikuu wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwamo za kitaaluma hivyo kamwe hatokubali kitumike kisiasa.

Akizungumzia uchaguzi huo ulifanyika mjini hapa ulishirikisha vyuo 35 kati ya 44 vinavyounda umoja huo, alisema ni umefanyika kihalali baada ya akidi kutimia na kwamba mgogoro uliokuwepo awali umekwisha baada kuvunjwa kwa makundi yaliyotokuwapo.

Awali Mwenyekiti wa Tume Uchaguzi Stanslauns Peter, alimtangaza John kuwashinda wagombea wenzake watano baada ya kupata kura 18 katika uchaguzi ulikuwa na upinzani mkubwa.

Nafasi ya Makamu mwenyeikiti ilichukuliwa na Tabia Maulid Mwita, Katibu Mkuu ilichaguliwa  na Leonald Kiongosi ,naibu wake Salum Hassan Salum huku Mweka Hazina aliyechaguliwa ni Alex Elifuraha na naibu wake Zainabu Ally Abdallah.
 
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

Previous Post Next Post