Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira.
Fedha hizo zinahusu ujenzi wa naabara za shule za sekondari inayotekelezwa katika vijiji vya Mihingo na Makomarito.
Fedha hizo zinazodaiwa kufanyiwa ubadhilifu zilitolewa na serikali, mfuko wa mbunge na michangi ya wananchi kwa ajili ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika vijiji hivyo.
Agizo la kufanyika kwa ukaguzi kuwabaini wajanja waliozitafuna fedha hizo yalitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mihingi, wilayani Bunda.
Waziri Wasira ambaye pia ni Mbunge wa Bunda, aliagiza ukaguzi huo ufanyika baaada ya kupokea malalamiko ya wananchi kwamba fedha za miradi ya maendeleo ya ujenzi wa maabara katika shule za sekondari za Mihingo na Makomarito zimeibwa.
Alisema kwamba ameelezwa na wananchi kuwa hali hiyo inawakatisha tama ya kuchangia nguvu zao katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Mheshimiwa umetoa Shilingi milioni mbili kwa ujenzi wa nyumba ya mganga, fedha hizo hazipo zimetafunwa. Hebu waulize kama zipo hapa hapa, hazipo wameshazila,” alisema mwananchi mmoja.
Kutokana na kauli hiyo, Wasira aliagiza ufanyike ukaguzi wa fedha hizo mara moja na kwamba iwapo itabainika kuwa zimetafunwa, wale wote waliohusika watachukuliwa hatua za kisheria.
“Tutaleta wakaguzi hapa ili wafanye ukaguzi wa fedha hizo tupate ukweli wa jambo hili, maana mimi kwenye mfuko wa mbunge nimetoa jumla ya Shilingi milioni mbili,” alisema waziri Wasira.
Kwa mujibu wa Wasira, katika ujenzi wa nyumba za mganga wa Kijiji cha Mihingo, licha ya wananchi kuchangia michango yao na serikali kutoa fedha nyingine, binafsi ameshachangia Sh. milioni mbili.
Wasira alisema katika ujenzi wa maabara katika Shule ya sekondari ya Mihingo, atachangia Sh. milioni moja na kuwataka viongozi wa kata hiyo kusimamia fedha hizo ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
CHANZO:
NIPASHE
إرسال تعليق