Watoto
53 wanaougua maradhi mbalimbali ya moyo wanaondoka leo kwenda India kwa
upasuaji. Watoto hao wanatarajiwa kuagwa na Makamu wa Rais, Dk.
Mohammed Gharib Bilal.
Taarifa iliyotolewa jana na Mratibu wa magonjwa ya moyo katika Klabu ya Lions ya Dar es Salaam, Dk. Rajni Kanabar, ilisema wagonjwa hao watatibiwa katika hospitali mbalimbali nchini India.
Alisema safari ya wagonjwa hao imeratibiwa kwa pamoja na Klabu ya Lions ya Dar-es-Salaam (Host), Regency Medical Centre na Wizara ya Afya ya Zanzibar.
Alisema katika kundi hilo, watakuwamo wauguzi wawili na madaktari wawili na wanatarajiwa kurudi nyumbani baada ya wiki nne zijazo.
Dk. Kanabar alisema wagonjwa 15 watatibiwa katika hospitali ya Jaypee Health Care Heart Institute iliyoko mji wa New Delhi na wengine 27 watatibiwa katika taasisi kubwa ya Fortis Escorts Heart iliyoko New Delhi, India.
"Watafanyiwa upasuaji ambao utagharimu Dola 2,500 za Marekani kwa kila mgonjwa na watapewa Dola 500 kwa ajili ya kujikimu wakiwa huko," alisema Dk. Kanabar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Hospitali ya Regency Medical Centre.
Alisema hospitali ya Ecorts ni miongoni mwa hospitali kubwa duniani kwa matibabu ya moyo na imekuwa ikiwafanyia upasuaji wagonjwa wa moyo kutoka Tanzania kwa punguzo kubwa la gharama za matibabu hayo.
Aliishukuru Wizara ya Afya ya Zanzibar kwa kuchangia nauli za ndege kwa wagonjwa 33 na kutoa Dola 500 kwa kila mgonjwa na Ubalozi wa India ambao viza za bure kwa wagonjwa wote kupitia balozi wa nchi hiyo hapa nchini, Debnath Shaw.
Dk. Kanabar aliwataja wengine waliochangia kuwa ni Bank M iliyochangia Dola 10,000 gharama za upasuaji wa wagonjwa wanne, Shirika la Nyumba na Klabu ya Lions Dar es Salaam (Host) Dola 16,500, Pradeep Kumar wa Bengaluru, India Dola 16,400, Regency Medical Centre Dola 12,500, wanafunzi wa British Columbia University Vancouver, Canada na Jumuiya ya Theosophical ya Dar es Salaam Dola 10,000.
Wengine ni Riyaz Hassan Ali wa Karim Foundation Marekani Dola 9,000, Familia ya Mohamed Gulam Dewji Dola 5,000, Africarriers Dola 5,000, Lakhan Pal wa Dar es Salaam Dola 2,500, Nashrin Sarkai wa Marekani Dola 5,000, Hazi Abbas wa Dar es Salaam Dola 2,500, Lion Siraz Jessa wa Dar es Salaam Dola 2,500, Lion Mohamed Laljee, Lion Yusuf Dalal, Lion Karim Meetha, Lion Nazmu Dola 3,500, Guru Sikh Sabha wa Dar es Salaam Dola 5,000, Harun Zacharia, Salim Turkey Dola 5,000, Dk. Kiran Nad Pallavi Patel wa Global Foundation Marekani Dola 10,000, Habib African Bank ya Dar es Salaam Dola 3,000 na Prem Kapoor & Family ya Mwanza Dola 3,000 na Gavana wa District 411B.

CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment