Watoto watatu wateketea kwa moto

Kamanda wa Polisi, mkoani Morogoro, Leonard Paulo.
Watoto watatu wamefariki dunia kwa kuungua na moto waliouwasha kwa lengo la kuwinda wanyama katika msitu wa mlima Migonjeni wilayani Kilosa, mkoani hapa.
Kamanda wa Polisi, mkoani Morogoro, Leonard Paulo, aliwataja watoto hao kuwa ni Rafael Bruno (7) mwanafunzi wa darasa la kwanza, Meshack Gasper (9), mwanafunzi wa darasa la tatu, wote wa Shule ya Msingi Mhubona na Juvens Bathoromeo (14).

Kamanda Paulo alisema ajali hiyo ilitokea juzi, saa 11 jioni wakati watoto hao walipowasha moto huo kwa lengo la kuzuia wanyama wasitoke katika eneo hilo ili wawakamate kirahisi.

Alisema moto huo uliwazunguka watoto hao na kushindwa pa kutokea.

Alisema kufuatia hali hiyo watoto hao waliungua hadi kufa papo hapo.
 
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

Previous Post Next Post