ZARI, DIAMOND MAHABA KWEUPE UGANDA

STORI: HAMIDA HASSAN na Musa Mateja
STAA anayetamba na ngoma mpya ya Nitampata Wapi, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mtoto mzuri kutoka Uganda, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wameoneshana malovee hadharani na kuwaacha watu midomo wazi.

Nasibu Abdul ‘Diamond’akiwa kwenye pozi na mtoto mzuri kutoka Uganda, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Tukio hilo lililoacha historia ya aina yake kwa kutokana na umaarufu wa wawili hao, lilitokea Jumatano iliyopita, nchini Uganda wakati Zari alipokwenda kumpokea Diamond katika Uwanja wa Ndege wa Kampala nchini humo.
‘Zari The Boss Lady ‘Diamond wakipata ukodaki.
Kwa mujibu wa chanzo kilichoambatana na Diamond, Zari alimpokea mgeni wake kwa mabusu motomoto na msafara wa kwenda hotelini ulipoanza, walipewa ulinzi mzito hadi hotelini ambako kila wakati wawili hao walipeana mabusu ya kiaina kuonesha ‘wamemisiana’.
Alipotafutwa Diamond kwa njia ya simu ya mkononi, hakutaka kufungukia mahaba hayo yaliyozua gumzo zaidi ya kucheka na kusema amejiandaa vilivyo kumpa sapoti Zari katika shoo yake ya All White Part iliyotarajiwa kufanyika juzi nchini humo.“Mwanangu nimejipanga, kitanuka mbaya katika hii shoo si unajua huwa sirudi nyuma?” alisema Diamond

Post a Comment

أحدث أقدم