Afa kwa kuchambuliwa na tembo wakiwinda wanyama

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga.
Mkazi wa Kijiji cha Kibutuka Wilaya ya Liwale mkoani hapa,  Mustafa Kinyuwile (40), amekufa papo hapo kwa kushambuliwa na tembo kwa kuvunjwa vunjwa mbavu na kunyofolewa jicho wakati na wenzake wakiwinda wanyama katika msitu wa Hifadhi ya Maliasili wa Selou.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga, alisema kuwa Kinyuwile alikumbwa na mkasa huo Desemba 31, mwaka jana mchana.

Mzinga alisema siku hiyo, Kinyuwile akiwa na wenzake wawili, walikuwa kwenye msitu huo wakifanya shughuli za uwindaji, ndipo tembo huyo aliyekuwa katika himaya yake aliwakimbiza na kumuua.

Akasema baada ya Kinyuwile kuuwawa na tembo huyo na aliondoka zake na mwili wake kuchukuliwa na wenzake hao na kuuacha eneo la kijiji cha Kilangala badala ya nyumbani kwake na wao kutokomoea kusikojulikana.

“Mwili wa huyu marehemu ulikutwa umetupwa eneo la kijiji cha Kilangala huku umenyofolewa jicho la kulia na mbavu zake zikiwa zimevunjwa vunjwa," alisema Mzinga.

Alisema uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa  wawindaji hao walikuwa wakifadhiliwa na mfanyabiashara wa vifaa vya pikipiki ambaye ni  ndugu watu aliokuwa akishirikiana na Kinyuwile katika shughuli zao za uwindaji.

Alisema  wanamshikilia mfanyabiashara huyo kwa mahojiano zaidi, huku akisubiri taratibu zingine za kisheria.

Post a Comment

Previous Post Next Post